News

Waziri Lukuvi apokea rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya ardhi nchini

Waziri Lukuvi apokea rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya ardhi nchini
Aug, 30 2018

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amepokea rasmi Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na Changamoto za Matumizi bora ya Ardhi Nchini na kutaja Teknolojia kuwa ni changamoto inayokabili mipango ya matumizi bora ya ardhi hali inayopelekea inayopelekea kulegalega kwa upangaji, upimaji na umikilishaji wa Ardhi.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo mjini Morogoro wakati alipokuwa akipokea rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za mipango ya matumizi bora ya ardhi nchini, iliyoonesha na kuainisha mapendekezo katika uandaaji,usimamizi na utekelezaji wa miapngo hiyo.

“Tunahitaji teknolojia rahisi ambayo hata ninyi mkiondoka serikali inaweza kuhimili, hatupendi mtuambukize teknolojia ambayo itakuwa ni ngumu kwetu, kwakuwa serikali inapopanga gharama kubwa zinajitokeza kwenye picha za anga na zile za chini,” alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema kuwa kuhusu fedha si tatizo lakini ukosefu wa teknolojia ndio tatizo kubwa zaidi,hivyo ni vizuri kuyatazama haya mashirika yasiyo ya kiserikali tushirikiane nayo ili yaweze kuangalia ni teknolojia gani rahisi itakayoweza kupunguza gharama za upimaji na upangaji wa ardhi vijijini baada ya kusubiri ndege za anga ambazo ni gharama kubwa.

Aliongeza kuwa Serikali inapenda kuwa na uratibu wa haraka, ulio rahisi ambao wananchi wanaweza kupanga maeneo yao pamoja na kuondokana na migogoro ya Ardhi ambayo imekuwa ikiibuka mara kwa mara kutokana na kukosekana kwa mipango ya matumizi ya ardhi.