Select Language:  ENGLISH   |   KISWAHILI

NLUPC Highlights

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akifungua Mkutano wa wadau wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini uliofanyika mwezi Agosti 2016 mjini Morogoro. Mheshimiwa Lukuvi aliwaagiza kuandaliwa kwa mafunzo ya uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ikiwemo miongozo na sheria za usimamizi wa ardhi kwa wanaosimamia ardhi nchini Mfano, Halmashauri za Wilaya, Vijiji na Viongozi katika ngazi mbalimbali n.k. Pia aliagiza kuwepo na uratibu wa uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini na kusisitiza kuwa Asasi za kiraia na wadau wengine wasiandae mipango ya matumizi ya ardhi bila kuwasiliana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ambayo ndiyo Mamlaka ya kusimamia na kuratibu mipango ya matumizi ya ardhi nchini. Alisema Tume itaelekeza maeneo ya kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi kulingana na malengo ya Serikali ili kupunguza migogoro.

Joomla! Debug Console

Session

Profile Information

Memory Usage

Database Queries