Select Language:  ENGLISH   |   KISWAHILI

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia za Care International-Tanzania, Jumuiko la Maliasili Tanzania na Oxfam Tanzania waliandaa na kuwezesha kufanyika kwa mkutano wa wadau wa siku mbili (2) kuanzia tarehe 4 hadi 5 ya Mwezi Agosti 2016 ili kujadili masuala yanahusu uratibu wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini. Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Wizara, Taasisi, pamoja na Asasi za Kiraia zinazojihusisha na masuala ya rasimlimali za ardhi.

Malengo ya mkutano huo ni pamoja na kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto na mapendekezo katika upangaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini. Pia mkutano huu ulilenga kuimarisha uratibu na ushirikiano baina ya sekta mbalimbali zinazohusiana na kupanga matumizi ya ardhi. Vile vile, mkutano huu ulilenga kujadili upangaji wa matumizi ya ardhi kama njia mojawapo ya suluhisho la migogoro ya ardhi na uwekezaji endelevu katika ardhi nchini.

Akifungua Mkutano huo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi alisisitiza kuandaliwa kwa mafunzo ya uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ikiwemo miongozo na sheria za usimamizi wa ardhi kwa wanaosimamia ardhi nchini Mfano, Halmashauri za Wilaya, Vijiji na Viongozi katika ngazi mbalimbali. Pia alisema lazima kuwepo na uratibu wa uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini. Mheshimiwa Waziri alisisitiza kuwa asasi za kiraia na wadau wengine wasiandae mipango ya matumizi ya ardhi bila kuwasiliana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ambayo ndiyo Mamlaka ya kusimamia na kuratibu mipango ya matumizi ya ardhi nchini. Tume itaelekeza maeneo ya kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi kulingana na malengo ya Serikali ili kupunguza migogoro. Mwishowe, Mheshimiwa Waziri alisisitiza umuhimu wa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya pamoja (Joint Land Use Plans); Pia, aliagiza mipango ya matumizi ya ardhi iandaliwe kwa awamu katika kila mkoa; na alipendekeza kuanza na Mkoa wa Morogoro ambapo vijiji vyote viandaliwe mipango ya matumizi ya ardhi; Kuwepo kwa takwimu sahihi za vijiji vyote vilivyoandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi nchini. Mipango ya matumizi ya ardhi iandaliwe hadi hatua ya Sita ili kusaidia jamii kukaa mahali pamoja na kuongeza tija katika shughuli zao za kiuchumi.

Baada ya majadiliano ya siku mbili, washiriki waliweka makubaliano yatakayohitaji utekelezaji kutoka katika taasisi mbalimbali na kuratibiwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi. Makubaliano hayo ni haya yafuatayo:

 1. Mkakati wa uratibu wa uandaaji, usimamizi mipango ya ya matumizi ya ardhi uliouhishwa na wadau ukamilishwe na uwezeshwe utekelezaji wake.
 2. Uandaliwe mkakati wa kufikia malengo wa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya wilaya 25 na vijiji 7500 kati ya mwaka 2015-2020.
 3. Uazishwe utaratibu wa kubainisha na kujumuisha kwa pamoja rasilimali fedha, utaalam kutoka kwa wadau kwa ajili ya kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi nchini
 4. Uandaliwe mpango wa kutoa mafunzo kwa wakufunzi juu ya mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuwe na utaratibu mmoja wa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi.
 5. Kuanzisha kanzidata ‘database’ itakayoonyesha idadi ya vijiji vyenye mipango ya matumizi ya ardhi, na njia ya kubadilishana taarifa za mipango ya matumizi ya ardhi baina ya wadau, na asasi za kiraia ili kujua walipo na kazi wanazofanya .
 6. Tume iwe na wawakilishi katika kanda watakao kuwa na jukumu la kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi katika kanda hizi.
 7. Mkakati wa mawasiliano wa Tume utafsiriwe na kuwekwa katika lugha rahisi na usambazwe kwa wadau.
 8. Tafiti za kisayansi ziangalie utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi na zihusishe matumizi ya ardhi ya asili (traditional land use practices).
 9. Kuwepo na mikutano ya wadau itakayojadili matokeo ya tafiti hizo na kurejea mipango ya utekelezaji.
 10. OR-TAMISEMI izielekeze Halmashauri za Wilaya kutenga bajeti kwa ajili ya kuandaa na kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi.
 11. Tume iandae mkakati wa uhamasishaji kwa viongozi na Watendaji Wakuu wa Halmashauri za Wilaya na Mikoa.
 12. Wadau wote pamoja na tujikite kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya pamoja (joint land uses).
 13. Vyombo vya habari vitumike katika kuhamasisha wadau wote (serikali, wahisani wa maendeleo, asasi za kiraia) kuongeza bajeti katika sekta ya ardhi hasa upimaji upangaji wa matumizi ya ardhi.
 14. Uandaliwe mkataba wa makubaliano baina ya asasi za kiraia juu ya ubadilishanaji wa taarifa za mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
 15. Wadau wa utekelezajii wa programu za mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi watafute fedha za kutekeleza programu hizo katika ngazi zao.
 16. Kiundwe kikosi kazi kitakachoratibu utekelezajii wa maazimio ya mkutano huu.

Joomla! Debug Console

Session

Profile Information

Memory Usage

Database Queries