Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: Tumeshikana na tumeimarika kwa maendeleo ya Taifa letu
Kikao Kazi cha Wadau wanaohusika na Uwezeshaji wa Uandaaji, Usimamizi na Utekelezaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi Nchini
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geofrey Pinda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namkatila wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda kukagua mradi wa upangaji mipango ya matumizi ya ardhi tarehe
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Malisili na Utalii Mhe, Timotheo Mzava akizungumza katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Namkatila katika hamashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi tarehe 13 Machi 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume Prof. Wakuru Magigi na Kamishna wa Uhifadhi wa TFS (waliokaa) wakitia saini makubaliano ya kuwezesha uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 14 vilivyopo kwenye safu ya Misitu ya Miombo katika Wilaya tatu, Mkoani Tabora
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua moja ya taarifa ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji cha Bulongwa, Wilayani Makete kabla ya kukabidhi Hati za Hakimiliki za Kimila kwa wananchi Wilayani humo
Mkurugenzi Mkuu wa Tume Prof. Wakuru Magigi akiwasilisha Mpango wa uendelezaji wa Vijiji vya Msomera, Kitwai na Saunyi wakati wa ziara ya kukagua kazi inayoendelea ya Upangaji Matumizi ya Ardhi kwa ajili ya wakazi wanaohamia kutoka Hifadhi ya Ngorongoro
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mh. Said Mtanda akizungumza na wataalamu kutoka Tume kabla ya kuanza kwa zoezi la uandaaji Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 64 vilivyopo katika Halmashauri za Wilaya ya Butiama, Musoma na Bunda Mkoani Mara.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo Mhe. Dkt. Angeline Mabula katika ofisi za Wizara eneo la Mtumba Jijini Dodoma
Mpima Ardhi wa Tume Emmanuel Mwanga akichukua majira nukta kwenye mpaka wa Vijiji vya Gomero na Kichangani, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakati wa zoezi la uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji jirani na Hifadhi ya Nyerere
Mtaalamu wa TEHAMA kutoka Tume, Bw. Gerald Mseti (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi namna Mfumo wa Taarifa za Matumizi ya Ardhi (National Land Use Information System – NLUIS) unavyofanya kazi katika utoaji wa Hati za Hakimiliki
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Makusi Wilayani Makete wakiwa kwenye Mkutano wa Kijiji kwa ajili ya kujadili na kupitisha mpango wa matumizi ya ardhi wa kijiji hicho
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Antony Mtaka (aliyesimama) akizindua Mkakati wa Kupanga, Kupima Ardhii na kutoa Hati Miliki za Kimila kwa wakulima wa ngano. jumla ya Vijiji 44 vinatarajiwa kuandalimwa mipango ya matumizi ya ardhi na kuandaliwa Hatimiliki
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kibuye, Kata ya Bukuba katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Mtaalamu kutoka Tume wakati wa Mkutano Mkuu kwa ajili ya uandaaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji hicho
Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Tume mara baada ya utambulisho wa uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 16 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime